Viwango vyetu
Ghetto ni ya watu wazima wanaotafuta, kupangisha au kusimamia nyumba. Lazima uwe na miaka 18 au zaidi kufungua akaunti. Haya hayaruhusiwi kabisa kwenye matangazo, picha, video, maoni, chat au wasifu:
- maudhui yoyote yanayowaonyesha watoto kingono au unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto;
- kumrubuni mtoto, au kujaribu kukutana na mtoto kwa nia ya kumnyanyasa;
- kusafirisha watoto kinyume cha sheria, au kutumia tangazo au nyumba kwa ajili hiyo.
Tunachofanya
- Tunaondoa maudhui na kufunga akaunti mara moja, bila onyo.
- Tunahifadhi ushahidi kama sheria inavyotaka na kuripoti kwa mamlaka za Tanzania.
- Tunashirikiana na polisi na mamlaka nyingine wanapochunguza.
Namna ya kuripoti
- Kwenye app: ripoti tangazo, mazungumzo au ujumbe (menyu, kisha Ripoti). Chagua sababu inayokaribia zaidi na ueleze kinachoendelea.
- Kwa email: mwandikie mtu wetu wa usalama wa watoto hapa chini. Huhitaji akaunti ya Ghetto.
Mtoto akiwa hatarini sasa hivi, piga simu polisi kwanza.
- Polisi na dharura
- 112
- Simu ya msaada kwa mtoto Tanzania, bure
- 116
Mtu wa kuwasiliana naye
Msimamizi wa usalama wa watoto, Solvitas Innovations Limitedghetto@solvitasinnovations.co.tz
Anajibu ripoti za usalama wa watoto na maombi kutoka mamlaka.
Kanuni zetu nyingine ziko kwenye miongozo ya jamii.