Ghetto ni mahali watu wanapotafuta, kupangisha na kusimamia nyumba na fremu za biashara. Miongozo hii inamhusu kila anayetumia app: wanaotafuta nyumba, madalali, wenye nyumba na wapangaji. Ni sehemu ya masharti ya matumizi.
Matangazo
- Tangaza nyumba au fremu iliyopo kweli, unayoimiliki au ambayo mwenye nyumba amekuruhusu kuipangisha.
- Picha na video ziwe za nyumba hiyo. Usitumie picha za nyumba nyingine au za mtandaoni.
- Bei, masharti, bili na gharama ya kuhamia ziwe sahihi.
- Ikichukuliwa, weka kuwa imechukuliwa mara moja. Ithibitishe tena app inapouliza.
- Nyumba moja, tangazo moja. Usiweke nyumba ileile zaidi ya mara moja.
- Usiweke masharti yanayowakataa watu kwa kabila, dini, jinsia au ulemavu.
- Usiombe pesa yoyote kabla mtu hajaona nyumba.
Maoni
- Unaweza kutoa maoni baada ya kuona nyumba au kuishi humo tu.
- Andika kuhusu nyumba na ulichopitia: hali yake, bili, na dalali au mwenye nyumba alivyokuhudumia.
- Usilipe maoni, usilipwe kuyaandika, wala usimshinikize mtu kuandika au kuondoa maoni.
- Usiandike maoni kuhusu tangazo au biashara yako mwenyewe.
- Usiweke namba za simu, anwani au taarifa binafsi za watu wengine. Hakuna matusi wala vitisho.
Chat
- Heshimu wengine. Hakuna matusi, unyanyasaji, vitisho wala ujumbe wa ngono.
- Hakuna spam, wala kutuma ujumbe uleule kwa watu wengi.
- Usiombe kodi, amana, ada ya kuona nyumba au ada ya booking kabla ya kuona nyumba na kusaini mkataba.
- Usishiriki taarifa binafsi za mtu mwingine bila ruhusa yake.
Mtu yeyote akikuomba pesa kabla ya kuona nyumba, usilipe. Ripoti mazungumzo hayo.
Wasifu
- Tumia jina lako halisi au jina la biashara yako, na picha au nembo yako mwenyewe.
- Mtu mmoja, akaunti moja. Usijifanye mtu mwingine, dalali mwingine au kampuni nyingine.
- Alama ya uthibitisho inaonyesha tumehakiki kitambulisho chako. Usiitumie kuonyesha kuwa Ghetto imekagua nyumba au makubaliano.
- Lazima uwe na miaka 18 au zaidi.
Hairuhusiwi kabisa
Hatuvumilii kabisa mambo haya. Tunaondoa maudhui na kufunga akaunti, bila onyo la kwanza.
- Maudhui yoyote yanayowaonyesha watoto kingono au kuwanyanyasa. Pia tunaripoti kwa mamlaka. Soma usalama wa watoto.
- Utapeli: matangazo ya uongo, kujifanya dalali au mwenye nyumba, kuchukua pesa kwa nyumba isiyopatikana.
- Vitisho vya vurugu, na chuki dhidi ya watu kwa kabila, dini, jinsia au ulemavu.
- Picha za uchi, na picha au ujumbe wa ngono.
- Kuuza au kutangaza chochote kilicho kinyume cha sheria.
Kuripoti
- Tangazo: lifungue, bonyeza menyu, kisha Ripoti tangazo hili. Chagua sababu, ongeza maelezo ukipenda, na utume.
- Mazungumzo: ndani ya chat, bonyeza menyu, kisha Ripoti.
- Ujumbe mmoja: ubonyeze na ushikilie, kisha Ripoti ujumbe huu.
- Maoni: yafungue, bonyeza menyu, kisha Ripoti maoni haya.
- Wasifu: ufungue, bonyeza menyu, kisha Ripoti wasifu huu.
- Kwenye tovuti: kila ukurasa wa tangazo na wasifu una kiungo cha Ripoti.
Timu yetu inaangalia kila ripoti ndani ya saa 24. Mtu unayemripoti haambiwi ni nani amemripoti, na anayeripoti hubaki bila jina kwake.
Kumzuia mtu
Mtu akikusumbua, mzuie. Fungua chat au wasifu wake, bonyeza menyu, kisha Zuia, au bonyeza Mzuie pia baada ya kutuma ripoti. Hataweza tena kukutumia ujumbe wala kuomba kuona nyumba zako, nawe huoni matangazo yake. Kumzuia hakuzuii maoni ya kuona nyumba, upangaji au kukaa ambako kulishatokea.
Watu uliowazuia wako kwenye Wasifu, chini ya Watu uliowazuia. Unaweza kuwaruhusu tena hapo.
Tunachofanya
Tunachofanya kinategemea kilichotokea na kama kimewahi kutokea kabla.
- Kuondoa maudhuiTangazo, maoni au ujumbe unaovunja miongozo hii unaondolewa.
- Kusimamisha tangazoWanaotafuta nyumba wakisema imeshachukuliwa, tangazo linasimamishwa hadi mwenye tangazo athibitishe kuwa bado iko wazi.
- Kukagua matangazo mapya kwanzaMwenye tangazo asipothibitisha mara 3 ndani ya siku 90, matangazo yake mapya yanakaguliwa kabla ya kuwekwa hewani.
- Kuondoa alama ya uthibitishoKwa wanaoendelea kuweka matangazo yaliyopitwa na wakati, ya uongo au yanayojirudia.
- Kusimamisha au kufunga akauntiKwa makosa yanayojirudia, na mara moja kwa jambo lisiloruhusiwa kabisa.
Ukiona tumekosea
Tukiondoa kitu, kukupa onyo au kusimamisha akaunti yako na unaona ni kosa, tuombe tuangalie tena kupitia arifa tunayokutumia. Unaweza pia kutuma email kwa ghetto@solvitasinnovations.co.tz ukitumia email au namba ya simu ya akaunti yako.
Omba ndani ya saa 72 baada ya uamuzi wetu. Mtu wa timu yetu analiangalia, pamoja na uamuzi uliofanywa kiotomatiki, kama tangazo lililoisha muda au onyo la kutothibitisha.
Wasiliana nasi
Maswali kuhusu miongozo hii yatumwe kwa ghetto@solvitasinnovations.co.tz. Kwa msaada mwingine, angalia Msaada.