Masharti haya yanahusu matumizi yako ya app ya Ghetto na tovuti hii. Ghetto inatolewa na Solvitas Innovations Limited (“sisi”), Dar es Salaam, Tanzania. Ukifungua akaunti au kutumia app, unakubali masharti haya na sera ya faragha. Kama hukubaliani nayo, tafadhali usitumie Ghetto.
Ghetto ni nini
Ghetto inasaidia watu kupata nyumba na fremu za biashara, madalali na wenye nyumba kuzitangaza, na wenye nyumba kusimamia upangishaji. Sisi si sehemu ya upangishaji, mauzo au makubaliano kati ya watumiaji. Sisi si dalali, wakala au mwenye nyumba, na hatumiliki, kukagua au kutoa dhamana kwa nyumba zinazotangazwa.
Akaunti yako
- Lazima uwe na miaka 18 au zaidi na utoe taarifa zako za kweli.
- Linda simu, email na kodi zako za OTP za kuingia. Unawajibika kwa kinachofanywa kupitia akaunti yako.
- Mtu mmoja, akaunti moja. Usiingie kama mtu mwingine au kuruhusu wengine kutumia akaunti yako.
Kutangaza kwenye Ghetto
Ukitangaza nyumba au fremu, unaahidi kwamba:
- wewe ni mmiliki au mwenye nyumba amekuruhusu kuipangisha;
- picha na video ni za nyumba hiyo, na bei, masharti, bili na gharama ya kuhamia ni sahihi;
- bado inapatikana. Ikichukuliwa, unaweka taarifa hiyo mara moja;
- unathibitisha tena inapoulizwa na app. Matangazo yasiyothibitishwa tena yanaisha muda wake.
Tunaweza kuficha, kusitisha au kuondoa tangazo, kuondoa alama ya uthibitisho, au kumsimamisha anayeweka matangazo yaliyopitwa na wakati, ya uongo au yanayojirudia.
Kutafuta nyumba
- Tembelea nyumba na uangalie mkataba kabla ya kulipa chochote.
- Usilipe kodi, amana au ada kabla ya kuona nyumba na kusaini mkataba. Ripoti yeyote anayekuomba ufanye hivyo.
- Alama ya uthibitisho inaonyesha tumehakiki kitambulisho cha mwenye tangazo. Haimaanishi tumekagua nyumba au makubaliano.
Madalali na wenye nyumba
Kamisheni yako na makubaliano yako na wateja na wenye nyumba ni kati yenu. Ghetto haichukui kamisheni yako. Ukisimamia wapangaji kwenye Ghetto, unawajibika kuwa na haki ya kuweka taarifa zao na kufuata sheria za upangishaji na taarifa binafsi.
Mambo yasiyoruhusiwa
- kuweka matangazo ya uongo, yanayopotosha, yanayojirudia, au ya nyumba usizoruhusiwa kupangisha;
- kuomba pesa kabla ya kuona nyumba, au kujaribu kutapeli, kutisha au kumsumbua mtu;
- kuwabagua watu kwa kabila, dini, jinsia au ulemavu;
- kuandika maoni kuhusu sehemu ambazo hujaziona au kuishi, au kulipia maoni;
- kunakili matangazo au taarifa nyingi kwa pamoja kutoka Ghetto, au kujaribu kuvunja usalama wake.
Mtu yeyote anaweza kuripoti tangazo, mazungumzo, ujumbe, maoni au wasifu kupitia app, na tangazo au wasifu kupitia tovuti. Hatuvumilii maudhui yasiyofaa: tunashughulikia ripoti ndani ya saa 24, na tunaweza kuondoa maudhui au kufunga akaunti zinazovunja masharti haya.
Kanuni kamili, na tunavyoshughulikia ripoti, ziko kwenye miongozo ya jamii. Unaweza kumzuia mtu yeyote kutoka kwenye chat au wasifu wake. Ukiona tumekosea uamuzi, tuombe tuangalie tena ndani ya saa 72 na mtu wa timu yetu atauangalia, pamoja na maamuzi yaliyofanywa kiotomatiki.
Maudhui yako
Matangazo, picha, video, ujumbe na maoni unayoweka vinabaki kuwa vyako. Unatupa ruhusa ya kuvihifadhi na kuvionyesha kwenye Ghetto, na kushiriki matangazo yako kwenye kurasa na chaneli unazochagua, kwa muda vinapokuwa kwenye Ghetto. App, muundo wake, jina na nembo ya Ghetto ni mali yetu.
Ada
Kutumia Ghetto ni bure wakati wa majaribio. Tukiongeza huduma za kulipia, tutaonyesha bei kabla hujalipa na kusasisha masharti haya kwanza.
Hakuna dhamana
Ghetto inatolewa “kama ilivyo”. Hatuahidi kuwa itapatikana kila wakati au haitakuwa na makosa, au kuwa kila tangazo, maoni au mtumiaji ni kama anavyoeleza.
Mipaka ya uwajibikaji wetu
Kwa kiwango kinachoruhusiwa na sheria, hatuwajibiki kwa hasara isiyo ya moja kwa moja au inayofuata kutokana na tukio, au hasara inayotokana na makubaliano, malipo au mkutano kati ya watumiaji. Masharti haya hayaondoi haki zako ambazo haziwezi kuondolewa chini ya sheria za kulinda watumiaji nchini Tanzania.
Mabadiliko na kusitisha matumizi
Tunaweza kusasisha app na masharti haya. Tukifanya mabadiliko makubwa, tutasasisha ukurasa huu na tarehe iliyo juu na kukujulisha kwenye app. Unaweza kuacha kutumia Ghetto wakati wowote na kufuta akaunti yako. Akaunti yako inafungwa papo hapo na kufutwa baada ya siku 30, na ukiingia kabla ya hapo ufutaji unasitishwa. Tunaweza kusimamisha au kufunga akaunti inayovunja masharti haya.
Sheria
Masharti haya yanafuata sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na migogoro inapelekwa kwenye mahakama za Tanzania.
Wasiliana nasi
Maswali kuhusu masharti haya yatumwe kwa ghetto@solvitasinnovations.co.tz.