Panga kwa usalama.

Utapeli mwingi wa nyumba unaanza na ombi la pesa kabla hujaiona nyumba.

Ghetto

Usilipe kodi, amana au ada kabla ya kuona nyumba na kusaini mkataba.

  1. 1Ione nyumba, ndani
  2. 2Soma na usaini mkataba
  3. 3Lipa, upate risiti
getghetto.app/safetyPanga kwa usalama

Utapeli wa aina tatu unaojulikana

  1. "Booking fee" kabla ya kuona nyumba

    Mtu anasema wateja ni wengi na anakuomba utume pesa kwa simu ili akushikilie nyumba. Ukishatuma, hapokei tena simu.

    Ishara
    Pesa inaombwa kabla hujaingia ndani, mara nyingi kwa haraka.
    Ufanye nini
    Usitume. Omba kuiona nyumba kwanza, na uripoti tangazo.
  2. Dalali au mwenye nyumba feki

    Mtu anajifanya dalali au mwenye nyumba, mara nyingi akitumia tangazo la mtu mwingine. Anakutana nawe karibu na nyumba, lakini hana funguo wala ruhusa ya kuipangisha.

    Ishara
    Hataki kutaja jina lake, anakwepa app, au hawezi kufungua mlango.
    Ufanye nini
    Fungua wasifu wake Ghetto na uangalie "Kitambulisho kimekaguliwa na Ghetto". Endelea na mazungumzo ndani ya app.
    Wasifu wa mwenye tangazo kwenye app. Wasifu wa mfano.
  3. Picha za nyumba nyingine

    Tangazo lina picha nzuri zilizochukuliwa mtandaoni au kwenye tangazo la mtu mwingine. Ukifika, nyumba ni tofauti, au haipo kabisa.

    Ishara
    Hakuna video, picha chache, na bei iko chini sana kuliko nyingine za eneo hilo.
    Ufanye nini
    Tafuta "Picha zilizothibitishwa": zimepigwa kwa kamera ya Ghetto kwenye pini ya nyumba. Ghetto inagundua picha iliyotumika kwenye tangazo la mtu mwingine.

Lipa baada ya kusaini, na uhifadhi risiti

Kodi mara nyingi inalipwa kwa miezi kadhaa kwa pamoja, kwa hiyo hakikisha mambo manne kabla ya kutuma pesa.

  • Umeingia ndani ya nyumba, si nje ya geti tu.
  • Unamjua mwenye nyumba, na dalali ana ruhusa ya kuipangisha.
  • Mkataba una jina la mwenye nyumba, kodi na miezi unayolipia.
  • Unapata risiti ya kila malipo.

Ghetto inachofanya

  • Kitambulisho kabla ya tangazo lolote

    Madalali na wenye nyumba hawawezi kuchapisha mpaka Ghetto ihakiki kitambulisho.

  • Picha zilizopigwa kwenye nyumba

    Picha za kamera ya Ghetto kwenye pini zinapata alama ya Imethibitishwa. Picha zilizotumika kwingine zinagunduliwa.

  • Maoni ya waliofika kweli

    Ni waliotazama au kupanga kupitia Ghetto tu wanaoweza kumpa mwenye tangazo maoni.

  • Matangazo yanayoisha muda

    Tangazo lisilothibitishwa linaondoka lenyewe. Jinsi matangazo yanavyobaki sahihi

  • Chat yenye kumbukumbu

    Ongea na wenye matangazo ndani ya app, na uripoti ujumbe wowote kutoka kwenye ujumbe wenyewe.

  • Ripoti zinaangaliwa na watu

    Timu yetu inaangalia kila ripoti na inaweza kuondoa matangazo na kufunga akaunti.

Alama ya uthibitisho inaonyesha tumehakiki kitambulisho cha mwenye tangazo. Haimaanishi tumekagua nyumba au makubaliano, kwa hiyo kanuni ya juu bado inafanya kazi.

Jinsi ya kuripoti

  1. Fungua tangazoBonyeza Ripoti, chini ya tangazo.
  2. Chagua sababuUtapeli, imeshapangishwa, taarifa au bei si sahihi, au limejirudia.
  3. Ongeza kinachotusaidia kuhakikiNamba iliyoomba pesa, kiasi, na tarehe.

Ujumbe kwenye chat: ubonyeze na kuushikilia, chagua Ripoti ujumbe huu, kisha Utapeli au ulaghai.

Jambo lililo nje ya app: tuma email kwa ghetto@solvitasinnovations.co.tz

Umeshatuma pesa? Piga simu kwa mtoa huduma wako wa pesa kwa simu mara moja, na uripoti polisi.

Madalali: watumieni wateja wenu ukurasa huu

Mteja anayejua kanuni hii anakuamini zaidi ukimwambia aje aone nyumba kwanza.

getghetto.app/safety

Tafuta nyumba kwa usalama

Nyumba na fremu za biashara Dar es Salaam, kwa Kiswahili na Kiingereza.