Wasiliana nasi
Tuandikie ukitumia namba ya simu au email ya akaunti yako, ili tuipate.
Wanaotafuta nyumba
-
Kila tangazo linaonyesha mara ya mwisho mwenye tangazo alipothibitisha kuwa bado ipo. Asipothibitisha Ghetto inapouliza, tangazo linaondoka lenyewe. Ukikuta imeshachukuliwa, iripoti kama “Imeshapangishwa au haipatikani”.
-
Hapana. Usilipe kodi, amana au ada kabla ya kuona nyumba na kusaini mkataba. Ripoti yeyote anayekuomba ufanye hivyo.
-
Ni unachalipa kuhamia: kodi ya miezi inayolipwa kabla, pamoja na ada ya dalali kama ipo. Kila bili pia inaonyesha kama imejumuishwa, mnachangia au unalipa peke yako.
-
Tumehakiki kitambulisho cha mwenye tangazo. Haimaanishi tumekagua nyumba au makubaliano, kwa hiyo ona nyumba na usome mkataba kabla ya kulipa.
-
Watu walioiona nyumba au kuishi humo kupitia Ghetto tu.
Madalali
-
Thibitisha kitambulisho chako kwanza: unahitaji kitambulisho kilichothibitishwa ili kuchapisha matangazo. Tangazo lako la kwanza linakaguliwa na timu yetu kabla halijawekwa hewani, mara nyingi ndani ya saa chache.
-
Hivyo ndivyo kila tangazo linavyobaki sahihi. Thibitisha matangazo yako tukikuuliza. Usipothibitisha mara 3 ndani ya siku 90, matangazo yako mapya yatakaguliwa kwanza.
-
Kwenye tangazo lako, fungua Shiriki tangazo hili na uchague ukurasa wako wa Facebook na channel yako ya Telegram. Kila tangazo lina link yenye taarifa za sasa: nyumba ikichukuliwa, inaonyesha nyumba zako nyingine zilizo wazi.
-
Hapana. Kamisheni yako na makubaliano yako na wateja na wenye nyumba ni kati yenu.
-
Kutumia Ghetto ni bure wakati wa majaribio. Tukiongeza huduma za kulipia, tutaonyesha bei kabla hujalipa.
Wenye nyumba
-
Ndiyo. Nyumba ikiwa wazi, itangaze kwa kubonyeza mara moja. Pangisha kupitia madalali wako, moja kwa moja au njia zote mbili.
-
Kila mpangaji anaonyesha tarehe aliyolipia hadi, kwa mzunguko wake mwenyewe. Vikumbusho vya kodi vinatumwa kwa niaba yako, na risiti zinatolewa zenyewe.
-
Hapana. Unaweza kumweka mpangaji kwa jina na namba ya simu, na vikumbusho vinamfikia kwa SMS. Mpangaji anayetumia Ghetto pia anaona mkataba, risiti na picha za hali ya nyumba yake.
-
Wewe, na wale unaowapa ruhusa. Tunazihifadhi kukusaidia kusimamia nyumba zako, na hatuzitumii kuwatangazia biashara wapangaji wako.
Ripoti tangazo au mtu
Tangazo la uongo, nyumba iliyokwisha chukuliwa, au mtu anayeomba pesa kabla ya kuona nyumba: tuambie kupitia tangazo hilo.
- Fungua tangazo na ubonyeze menyu.
- Chagua Ripoti tangazo hili.
- Chagua sababu na uongeze maelezo ukipenda.
- Bonyeza Tuma ripoti. Timu yetu inaliangalia ndani ya saa 24.
Ndani ya chat, bonyeza menyu na uchague Ripoti. Kuripoti ujumbe mmoja, ubonyeze na ushikilie.
Huna app? Tuma link ya tangazo kwa ghetto@solvitasinnovations.co.tz. Tunachoshughulikia kiko kwenye miongozo ya jamii.
Futa akaunti yako
Kwenye app: Wasifu, Badilisha, kisha Futa akaunti chini ya Taarifa binafsi. Kama huna app tena, tuma ombi kupitia tovuti.